Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli jana amewasili mkoani Kilimanjaro ambapo atafanya ziara ya kikazi kwa muda wa siku tatu.

Pia Rais Magufuli anatarajiwa kuhudhuria sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ambapo atakuwa mgeni rasmi.

Rais amewasili mkoani humo ikiwa ni siku moja baada kupokea ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma ambapo watumishi 9,932 aliwatimua kazi baada ya kubainika kuwa wamegushi vyeti.

Katika ziara yake hiyo akiwa njiani Rais John Magufuli  amewaambia wakazi wa mji wa Bomang’ombe katika Jimbo la Hai kuwa amewasamehe kutokana na kutomchagua kwenye uchaguzi uliopita.

Alitoa kauli hiyo akiwa katika jimbo hilo la Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe baada ya kuwaona baadhi ya wananchi wakiwa wameshika jani la “Sale” ambalo hutumiwa na wenyeji kuomba msamaha.

 

Jani hilo linaloheshimiwa sana na wachaga wa mkoa huo, ndilo ambalo mtu akimpelekea mtu aliyemkosea na kumuomba yaishe, anayeombwa kupitia jani hilo hana jinsi lazima akubali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *