Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kote nchini na kuwataka kuwa na nidhamu ya pesa na kutumia fedha za serikali vizuri.

Rais Magufuli amesema hayo leo wilayani  Chato mkoani Geita alipokuwa akihutubia wananchi katika makabidhiano ya nyumba 50 zilizojengwa na taasisi ya Benjamin Mkapa  mkoani humo.

Pia Rais Magufuli aliwataka wananchi wa hali ya chini kuwa na amani kwani katika kipindi chote ambacho yeye atakuwa madarakani hataki kuona wala kusikia wananchi wa hali ya chini wakinyanyaswa.

Rais Magufuli amesema kuwa hataki kuona wananchi wa hali ya chini wananyanyaswa kwasababu na yeye ametokea katika maisha hayo hivyo anatambua jinsi wanavyopata shida watu wa kipato cha chini.

Rais Magufuli akuziacha taasisi ambazo zimekuwa zikitetea wanafunzi kupata mimba na kusema yeye taasisi hizo hazipendi na ameziwekea kizingiti kuwa ikiwezekana zisipewe msaada bali taasisi zinazofanya mambo ya kimaendeleo kama taasisi ya Mkapa Foundation ndiyo zinatakiwa kupewa msaada sana kwa kuwa zinarudi kuleta maendeleo kwa wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *