Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaambia wabunge wa CCM kuwa anamuunga mkono Waziri mkuu, Kassimu Majaliwa hata kama wao wanampinga.

Pia Rais Magufuli amewaonya wabunge wa chama hicho wanaotoa muda wa kuchangia bungeni kwa wapinzani huku akieleza na tabia ya baadhi ya wabunge wanaopinga vita dhidi ya dawa za kulevya.

Rais Magufuli ameongea hayo jana mkoani Dodoma Ikulu ndogo ya Chamwino ambapo amesema yeye ndiyo aliyamua bunge kutooneshwa moja kwa moja katika Television.

Kikao hicho cha wabunge wa CCM kimefanyika baada ya siku chache kumalizika kwa kikao cha Chama hicho na kupitisha mabadiliko ya katiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *