Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaapisha Mawaziri na Manaibu Mawaziri wapya walioteuliwa kufuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Oktoba 7 mwaka huu.

Hafla ya uapishaji inafanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam na imehudhuriwa na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali, Bunge na Mahakama kwa ujumla.

Baadhi ya mawaziri na manaibu waliokula kiapo leo ni wale walioteliwa kushika nafasi hizo siku ya Jumamosi baada ya mabadiliko madogo ya baraza hilo.

Baraza hilo la mawaziri kwasasa linakuwa na wizara 21 kutoka 19 baada ya kuongezeka kwa wizara mbili ambazo ni wizara ya wizara ya nishati ambayo imegawanjwa kutoka wizara ya nishati na madini.

Huku wizara ya Kilimo ikiwa peke yake baada ya kugawa kutoka wizara ya kilimo, uvuvi na mifugo.

Manaibu waziri nao wameongezeka mpaka kufika idadi ya manaibu waziri kufikia 21 ambapo wameongezeka manaibu watano.

Baada ya kuapishwa Rais Magufuli amewataka Mawaziri hao kuanza kazi mara moja, na wamebadilishana nyaraka mbali mbali za wizara ambazo walikuwa wanatumikia awali, kwa wale ambao wamehamishwa wizara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *