Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji mmoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa moja ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.

Wakurugenzi walioteuliwa ni kama ifuatavyo Godwin Kunambi(Manispaa ya Dodoma), Elias Ntiruhungwa(Mji wa Tarime), Mwantumu Dau( Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba).

Pia amewateua Frank Bahati (Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe), Hudson Kamoga (Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu), Mwailwa Pangani (Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo).

Wengine ni Godfrey Sanga(Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama), Yusuf Semuguruka(Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga), Bakari Mohamed(Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea).

Pamoja na Juma Mnwele(Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo), Butamo Ndalahwa(Halmashauri ya Wilaya ya Moshi), Waziri Mourice( Halmashauri ya Wilaya ya Karatu) na Fatma Latu( Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *