Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Emmanuel Mkumbo.

 Taarifa ya Ikulu jijini Dar es Salaam imesema Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkumbo kuanzia leo Oktoba 18.

Uteuzi wa Mkurugenzi mpya atakayejaza nafasi hiyo utatangazwa hapo baadaye baada ya kuchaguliwa.

Mkurugenzi huyo aliyetumbuliwa kwa sasa anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumtishia bastola askari wa kike wa usalama wa barabarani (Traffic).

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *