Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) Dkt. James Munanka Wanyancha.

Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia leo na amemteua Joseph Odo Haule kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo.

Uteuzi wa Joseph Odo Haule umeanza leo kabla ya uteuzi huo Joseph Odo Haule alikuwa Meneja wa Mfuko wa Barabara (Road Fund).

Wajumbe wengine wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wanaendelea katika nafasi zao kama kawaida.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *