Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametaka ujenzi wa Barabara za juu (Ubungo Interchange) kukamilika kabla ya miezi 30 muda ambao mkandarasi apewa na Serikali.

Barabara hiyo itajengwa na mkandarasi wa kampuni ya China ya CCECC kwa sh.188.7 bilioni ambapo Benki ya Dunia itatoa sh.186.8 bilioni huku Serikali ikitoa sh.1.9 bilioni kwa ajili ya ujenzi huo.

Ujenzi wa barabara hiyo umezinduliwa jana na Rais Magufuli akiwa na rais wa Benki ya Dunia,  Dkt. Jim Yong Kim eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo unatarajiwa kukamila Sepetemba mwaka 2019.

Rais Magufuli ameongeza kwa kusema kuwa hakuna haja ya mkandarasi kuchelewesha ujenzi huo kwasababu fedha za kutosha zipo kwa hiyo umalizike hata ndani ya miezi 20.

Pia Rais Magufuli amewataka wananchi walipe kodi ili Serikali iweze kulipa deni la benki ya Dunia waliokopa kwa ajili ya Barabara hiyo pamoja na kuendeleza miradi mengine.

Uzinduzi wa uwekaji jiwe la msingi wa barabara hiyo pia umehudhuriwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na viongozi wengine.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *