Hip Hop ya Bongo imemaliza ‘madongo yake’ kwa utawala wa Serikali?

Unadhani mastaa wangapi wa HIP HOP bado hawajaachia ‘vigongo’ vyao kwa Serikali ili kuikumbusha na kuirekebisha?

Mmoja kati ya mastaa ambao walipata sifa kubwa kwa kuukosoa utawala wa awamu ya nne uliokuwa chini ya Dkt. Jakaya Kikwete ni Roma ambaye ameahidi kuachia ‘dongo’ kwa utawala mpya.

Sambamba na Roma, kauli ya Nay wa Mitego ya kuwataka wasanii wa HIP HOP wasijisahau kwani siasa inaweza kuumeza muziki imewafanya waliokuwa mafichoni nao kuonyesha hamu ya kutaka kusema neno.

Weusi wameachia ngoma YA KULEVYA inayotajwa kuwa ni kazi ya fasihi inayokosa utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wa sasa na pia staa wa zamani wa kundi la WAGOSI WA KAYA, Mkoloni ameachia ngoma ya DEREVA.

Mapema mwaka huu, ngoma ya Nikki Mbishi ‘I AM SORRY JK’ ilifungiwa na BASATA kwa kukosa maadili.

Unadhani Profesa Jay, Mfalme Afande Sele, Bonta na mastaa wengine watafumbua midomo yao sasa baada ya ngoma ya Nay kupewa BIG UP na rais?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *