Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa  amesitikishwa na gharama kubwa ya ujenzi wa jengo jipya kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA).

Dkt. Magufuli amesema hayo alipofanya ziara ya ghafla katika uwanja huo wa ndege kwa ajili ya kwenda kuangalia ujenzi unaoendelea katika uwanja wa ndege huo wa kimataifa wa Mwalim Julius Nyerere.

Gharama hiyo ni ya shilingi bilioni 590, ambayo ni kubwa ikilinganisha na jengo lililojengwa katika uwanja huo.

Awali mkandarasi anayejenga uwanja huo ambaye ni kampuni ya BAM International , alitangaza kusitisha ujenzi huo kutokana na kutolipwa. Mheshimiwa Rais Magufuli aliahidi kulipa fedha hizo.

Rais Magufuli amemuagiza waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof Makame Mbarawa kuunda timu ya wataalamu watakaofanya tathimini ya utekelezaji wa mradi huo.

Pamoja na kuzungumza na mkandarasi anayejenga uwanja huo na Mhandisi mshauri ambao wamekubali kupunguza gharama za ujenzi wa mradi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *