Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa amesikitishwa na yaliyotokea kwenye ripoti ya pili ya mchanga wa madini iliyowasilishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais Magufuli amezungumza kwa uchungu kuhusu ripoti hiyo, na jinsi Watanzania wanavyoendelea kuteseka kwa umaskini wakati rasilimali zao zikisafirishwa nje ya nchi kwa njia zisizo halali.

Ripoti hiyo imewasilishwa na kamati ya uchunguzi wa usafirishaji wa mchanga wa madini (Makinikia) Prof. Nehemia Eliachim Ossoro ambapo rais ameonesha kuhuzunishwa na kukasirishwa na kilichomo kwenye ripoti hiyo.

Ripoti ya kamati hiyo, inakuja siku chache baada ya kamati ya kwanza iliyoongozwa na Profesa Mruma, nayo kukabidhiwa kwa mheshimiwa Rais, ikionesha ubadhirifu mkubwa wa rasilimali za taifa, katika sekta ya madini nchini.

Kamati hiyo imebainisha kuwa kupitia hati ya usafirishaji wa melini, idadi kubwa ya makontena yalikuwa yakisafirishwa bila kuorodheshwa.

Idadi na uzito wa makontena ya mchanga ulionekana kuwa mkubwa kwenye meli tofauti na kwenye nyaraka za bandarini.

Bulyanhulu na Pangea wamekuwa wakiuza makinikia nje ya nchi kinyume na taratibu za nchi kuhusu madini hayo.

Pia Kamati imebaini kuwa Acacia Mining PLC inafanyakazi za uchimbaji wa madini nchini kinyume na sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *