Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amemuapisha, Brigedia Jenerali, John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.

Sherehe ya kuapishwa kwa kiongozi huyo imefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Brigedia Jenerali John Julius Mbungo akila kiapo cha maadili ya Viongozi wa serikali baada ya kumuapisha kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.

Tukio hilo la kuapishwa kwa kiongozi huyo limeudhuriwa na viongozi wa Serikali akiwemo waziri wa Katiba na Sheria, Palamagamba Kabudi pamona na waziri wa Utumishi wa Umma, Angela Kailuki.

Viongozi wengine walioudhuria sherehe hiyo ni Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa majeshi ya Ulinzi nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *