Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli leo amemuapisha Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika ghafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam iliyohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kitaifa wakiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Majaji wengine wa Tanzania.

Baada ya kula kiapo Jaji Ibrahim Juma amesema anashukuru kwa kurasimishwa kushika wadhifa huo, ambao alikuwa ana ukaimu takriban miezi nane mpaka alipoteuliwa kuwa Jaji Mkuu.

Katika hotuba yake ya kwanza Jaji Mkuu Ibrahi Juma ameahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa weledi ikiwemo kulinda sheria na kuweka imani kwa wananchi, kwani wao ndiyo watetezi wao.

Ibrahim Juma alianza kutumikia wadhifa wa Kaimu Jaji Mkuu tokea Januari 18 mwaka 2017, baada ya aliyekuwa Jaji Mkuu wa nchi Mheshimiwa Mohamed Chande Othman kustaafu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *