Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemuapisha kamishna wa polisi    Diwani Athuman Msuya kuwa katibu Tawala wa mkoa wa Kagera.

Hafla ya kuapishwa kwa kamishna huyo imefanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali akiwemo waziri wa TAMISEMI, George Simbachawene.

Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Jaji mkuu Othuman Chande, Mwanasheria mkuu wa Serikali, George Masaju pamoja na Mkuu wa Jeshi la polisi IGP, Ernest Mangu.

Kamishna Diwani Athuman Msuya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Amantius Msole ambae uteuzi wake ulitenguliwa na rais mwezi uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *