Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli jana alimuandalia dhifa ya kitaifa mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Lungu iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Dhifa hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa ilihusisha viongozi mbalimbali wa sasa na wastaafu, huku pia wakialikwa wafanyabiashara, watendaji wa serikali, viongozi wa vyama vya siasa, mabalozi na watu wengine mashuhuri.

Viongozi waliohduria dhifa hiyo ni Rais Mstaafu wa awamu ya Pili AlhajAli Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume.

Wengine ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *