Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt. Mwele Malecela.

Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR atakayejaza nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Mwele Malecela utatangazwa baadaye.

Dk Mwele alinukuliwa na vyombo vya habari akizungumza kuhusu uwepo wa ugonjwa wa ZIKA Tanzania na kwamba asilimia 15 ya waliopimwa walikutwa na virusi vya ugonjwa huo ambapo hata hivyo taarifa hizo zilikanushwa na wizara ya afya jana.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *