Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), Uledi Mussa mjini Dodoma jana.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema hatua ya utenguzi huo ni kutokana na kutozingatiwa kwa taratibu zinazotakiwa katika kushughulikia masuala ya uwekezaji.

Mr. Uledi Mussa: Katibu mkuu wa ofisi ya waziri mkuu (Bunge) aliyetumbuliwa na Rais Magufuli.
Mr. Uledi Mussa: Katibu mkuu wa ofisi ya waziri mkuu (Bunge) aliyetumbuliwa na Rais Magufuli.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa utenguzi huo pia umefanyika ili kupisha uchunguzi wa ukiukwaji huo wa taratibu za uwekezaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *