Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amemteua Jenerali Mstaafu George Waitara kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa).

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza toka juzi jumamosi.

Pia, Rais Magufuli amemteua Dk Eligy Shirima kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (Taliri)
Uteuzi wa Dk Shirima nao umeanza jana.

Kabla ya uteuzi huu Dk Shirima alikuwa Mtafiti Mkuu na Msimamizi wa Utafiti wa Nyama ya Ng’ombe Makao Makuu ya Taliri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *