Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Raphael Chibunda kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam jana imeeleza kuwa uteuzi wa Profesa Chibunda umeanza jana.

Profesa Chibunda kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Sayansi na Teknolojia katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia.

Profesa Raphael Chibunda anachukua nafasi ya Profesa Gerald Monela ambaye amemaliza muda wake.

Kwa upande mwingine Rais Magufuli amewasili mjini Dodoma ambako pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

 

Sherehe hizo za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka huu zinafanyika mkoani Dodoma ambapo ndiyo makao makuu ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *