Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko ya uongozi kwa kumteua Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Waziri mkuu amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha ambapo anatarajiwa kuapishwa kesho saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *