Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Doto M. James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango akichukua nafasi ya Dkt. Servacius Likwelile.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Doto M. James alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera).

Bw. Doto M. James anatarajiwa kuapishwa kesho tarehe 01 Septemba, 2016 saa 2:45 Asubuhi katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 Kufuatia uteuzi huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile atapangiwa kazi nyingine.

 

Ikulu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *