Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Abdallah Possi kuwa Balozi.

Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Dkt. Abdallah Possi itatangazwa baadaye.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Abdallah Possi alikuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu aliyekuwa akishughulikia Ulemavu.

Kufuatia uteuzi wa Dkt. Abdallah Possi kuwa Balozi, nafasi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu (Ulemavu) itajazwa baadaye.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *