Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amemteua Andrew Wilson Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Kabla ya uteuzi huo Bw. Andrew Wilson Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu Tanzania (BOT).

Bwana Massawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Modestus Kipilimba ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

uteuzi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *