Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo kujitathmini na kuachia ngazi nafasi yake.

Hayo yamejiri baada ya Rais Magufuli kupokea ripoti ya uchunguzi kuhusu mchanga wa dhahabu uliopo katika makontena hapa nchini.

Pia Rais Magufuli amemfuta kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), na kuivunja bodi hiyo kwa upotevu wa madini.

Rais Magufuli ameitaka TAKUKURU na vyombo vya dola kuwachunguza na kuwachukulia hatua wafanyakazi wa bodi hiyo.

Rais Magufuli ameonesha kusikitishwa mno na ripoti hiyo ambayo imebainika kwamba kiwango kikubwa cha madini kinachotoroshwa nje ya nchi.

Mwisho Rais Magufuli ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinalinda madini yasitoroshwe na amepiga marufuku usafirishwaji wa mchanga huo nje ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *