Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) Archado Mtalemwa ajiandae kustaafu kutokana na mapungufu mengi ambayo Rais amesema ameyaona katika mamlaka hiyo.

Rais ameyasema hayo jana akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani na alitumia fursa hiyo kuzungumzia miradi ya maji na ulipaji wa maji kwa taasisi za serikali.

Rais Magufuli amesema kuwa “Ndugu yangu Mtalemwa, naongea kwa lugha nzuri hapa, nikuombe tu kuwa ustaafu mapema, inawezekana Waziri wa Maji ni rafiki yako, kama ilivyo kwa mawaziri wengine, lakini nadhani huu ni wakati mzuri,”.

Akizungumzia kuhusu deni la shilingi bil 40 ambazo taasisi mbalimbali za serikali zinadaiwa na idara ya maji  Rais Magufuli ametaka taasisi hizo zikatiwe maji mpaka pale zitakapolipa madeni yake.

Pamoja na hayo Rais amemshukuru Waziri Mkuu wa India kwa kutoa kiasi cha shilingi tril 1.3 kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maji katika mikoa 16 nchini pamoja na kumhakikishia Balozi wa India kuwa mahusiano kati ya nchi hizo yataendelea kuimarika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *