Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza rais wa Rwanda kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo kwa muhula wa tatu mfululizo.

Kagame ametangazwa mshindi wa Urais wa nchi hiyo baada ya kushinda katika uchaguzi Mkuu uliofanyika  August 4, 2017 na kumrudisha madarakani kwa muhula wa tatu.

Baada ya ushindi huo Rais wa Tanzania John Magufuli ametumia ukurasa wake twitter kumtumia salamu za pongeni Rais Kagame.

”Nakupongeza Mhe. Paul Kagame kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Rwanda kwa kipindi kingine. Kwa niaba ya Watanzania wote nakutakia mafanikio mema.

“Tutaendeleza na kukuza zaidi ushirikiano na uhusiano kati ya nchi zetu hususani biashara na maisha ya wananchi wetu. Hongera Wanyarwanda.”

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *