Rais Magufuli amezitaka TBS, TFDA na TRA kufanya kazi masaa 24 bandarini

0
313

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru taasisi zinazofanya kazi na Mamlaka ya Bandari(TPA), zikiwamo Shirika la Viwango(TBS), Mamlaka ya Chakula(TFDA), Mamlaka ya Mapato (TRA) na kampuni za uwakala wa forodha, kufanya kazi saa 24 ili kuondoa ucheleweshaji wa mizigo.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC).

Amesema haiwezekani Bandari ya Dar es Salaam itumie siku 14 kutoa mzigo wakati Mombasa inatumia siku tatu hadi nne tu.

Magufuli alifikia uamuzi huo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania Tatoa), Angelina Ngakula, kwamba taasisi hizo zimekuwa zikichangia katika ucheleweshaji wa mzigo na kujikuta wanatumia hadi wiki mbili kupakia mizigo yao.

Amesema wamejikuta wanapoteza muda mwingi kwenye Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kukosekana kwa ushindani hivyo kupoteza soko la tani milion tatu katika nchi nyingine kutokana na ucheleweshaji huo.

Pia Angelina alisema kukosekana kwa tani hizo kunaikosesha serikali Sh. trilion moja kutokana na wateja kuogopa kutumia bandari hiyo kwa kuhofia ucheleweshaji.

LEAVE A REPLY