Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewasili Mkoani Dodoma ambako pamoja na mambo mengine ataongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

Pia Rais Magufuli ataongoza mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi.

Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM ataongoza kikao na mikutano hiyo kuanzia tarehe 10 – 12 Machi, 2017 Mjini Dodoma.

 

Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wamewasili katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma akitokea Mkoani Morogoro ambako alizindua uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *