Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha viongozi mbalimbali kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam mapema hii leo.

Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na wake wa vikosi vya ulinzi na usalama wa nchi.

Jumla ya viongozi wapya sita wakiwemo mabalozi wameapishwa hii leo. Walioapishwa ni:

Prof. Palamagamba Aidan Kabudi – Waziri wa Katiba na Sheria

Alfayo Kidato –  Katibu Mkuu Ikulu

Sylvester Mabumba – Balozi Comoro

Abdallah Possy – Balozi Ujerumani

George Masima – Balozi Israel

Stella Mgasha – Kamishna wa Tume ya Utumishi na Mahakama

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *