Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameteua kamati ya wataalamu watakaofanya uchunguzi kwa lengo la kubaini kiwango cha madini kilichomo katika makontena yenye mchanga wa madini yanayoshikiliwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kamati hiyo yenye wajumbe 8, inatakiwa kuanza kazi haraka iwezekanavyo.

Wajumbe hao ni

  1. Abdulrahman  Hamis Mruma
  2. Justianian Rwezaura Ikingula
  3. Joseph Bushweshaiga
  4. Yusuf Ngenya
  5. Joseph Yoweza Philip
  6. Ambrose Itika
  7. Mohamed Zengo Makongoro
  8. Hery Issa Gombela

Wajumbe wote wa kamati hii wanatakiwa kufika ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam kesho Ijumaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *