Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amepokea hati za utambulisho wa mabalozi sita watakaowakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi hao ambao hati zao zimepokelewa na Rais Maguli ni kutoka Saud Arabia, Mohamed Bin Mansour Al Malek, Balozi wa Morocco, Abdelilah Benryane, Balozi wa Zambia, Benson Keith Chali.

Wengine ni Balazo wa Cuba, Lucas Domingo Hernandez Polledo, Balozi wa Iran, Mousa Farangh na balozi wa Burundi, Gervais Abayeho.

Baada ya kupokea hati zao Rais Magufuli amewakaribisha mabalozi hao hapa nchini na kuwahakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikina na nchi hizo katika nyanja mbali hasa za kiuchumi.

Kwa upande wa mabalozi hao wamempongeza Rais Magufuli kwa hatua anazochukua kujenga uchumi wa Tanzania kwa kukabiliana na rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na kusimamia uwajibikaji wa viongozi na watumishi wa umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *