Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amemuapisha Thobias Andengenye kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Andengenye anachukua nafasi ya Kamishna Jenerali Pius Nyambacha ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.

Pia Rais Dk. Magufuli amewaapisha mabalozi wanne walioteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali ambako Dk. Pindi Chana ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya kuchukua nafasi ya John Haule ambaye amestaafu.

Silima Kombo Haji ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Khartoum, Sudan ambako anakwenda kufungua Ubalozi huku Abdallah Abas Kilima akiapishwa kuwa Balozi wa Tanzania, Muscat, Oman ambako anachukua nafasi ya Ali Ahamed Saleh aliyestaafu.

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao ilihudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *