Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli leo amewaapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo kushika wadhifa huo, akichukua nafasi ya Mwamunyange aliyestaafu.

Katika hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ikulu pia Rais Magufuli amemuapisha pia Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa na Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali James Mwakibolwa.

Pia Rais Magufuli amewaapisha Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Samwel Shelukindo na Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Paul Meela.

Kwa upande mwingine Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna wa Polisi, Ernest Mangu amemuapisha Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *