Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kusitisha kuwapa uraia wa Burundi kuanzia sasa.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akiwahutubia wakazi wa Ngara mkoani Kagera ambapo alitembelewa na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza.

Magufuli amemtaka waziri Nchemba kusitisha kuwapa uraia waburundi kutokana na nchi hiyo kwasasa kuwa na amani tofauti na hapo nyuma.

Akizungumza baada ya kuwasili wilayani Ngara leo mkoani Kagera, Rais Nkurunziza amesema kuwa kwasasa nchi hiyo ina amani huku akiwaomba raia wa nchi hiyo walio Tanzania kurejea nchini kwao.

Rais Nkurunziza amesema kuwa anawataka wananchi wa Burunid kurejea ili kujenga nchi yao kwani sasa amani imerejea kama zamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *