Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli  amemteua Rogers William Sianga kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (Drug Control and enforcement Authority).

Kamishna Mkuu Rogers William Sianga atasaidiwa na Mihayo Msikhela ambaye anakuwa Kamishna wa Operesheni na Fredrick Kibuta anakuwa Kamishna wa Intelijensia.

Kwa upande mwingine Rais Magufuli amemteua Dkt. Anna Peter Makakala kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Anna Peter Makakala alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji Moshi kilichopo Mkoani Kilimanjaro.

Uteuzi huu unaanza mara moja na wateule wote wataapishwa Jumapili tarehe 12 Februari, 2017 saa 5:00 Asubuhi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *