Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amelaani mauaji ya askari polisi nane yalitokea usiku wa kuamkoa leo katika eneo la Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.

Katika taarifa iliyototolewa na Kurugenzi ya Ikulu imesema kuwa Rais Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Askari hao.

Askari Polisi hao walikuwa wakitoka kubadilishana doria na wameshambuliwa kwa kupigwa risasi wakiwa wanasafiri kwa gari katika barabara ya Dar es Salaam – Lindi.

Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP-Ernest Mangu, familia za askari wote waliouawa, Askari Polisi wote na Watanzania wote walioguswa na vifo hivyo.

Magufuli amelaani tukio hilo na matukio yote ya kuwashambulia askari polisi ambao wanafanya kazi kubwa na muhimu ya kulinda raia na mali na ametaka Watanzania wote watoe ushirikiano katika kukomesha vitendo hivyo.

Rais Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *