Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi watatu, wawili wakiteuliwa kuwa wabunge huku mmoja akiteuliwa kuwa balozi.

Walioteuliwa na Rais Magufuli kuwa wabunge ni Alhaji Abdallah Majula Bulembo pamoja na Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi ambao wataapishwa kwa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia Rais Magufuli amemteua Benedicto Martin Mashimba kuwa balozi ambaye atapangiwa kituo cha kazi hapo baadae.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *