Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kuachiwa  huru kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ney wa Mitego na wimbo wake ‘Wapo’ uchezwe kwenye media mbalimbali hapa nchini.

Rais Magufuli amesema amefurahishwa na wimbo huo ‘Wapo’ huku akimshauri mwanamuziki huo kutaja majina ya watu wengine kwenye wimbo huo kama vile wakwepa kodi, wauza unga, wabwia unga na watu wengine wasiokuwa na maadili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma leo.

Pia Mwakyembe amelishauri Jeshi la Polisi nchini kumuachia huru mwanamuziki huyo kutokana na kutokuwa na makosa.

Mwakyembe amewataka BASATA kuondoa agizo lake dhidi ya wimbo na badala yake uendelee kupigwa kama nyimbo nyingine.

Nay wa Mitego alikamatwa mkoani Morogoro baada ya kuachia wimbo wenye kuikashifu Serikali iliyopo Madarakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *