Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na waziri wa Maendeleo wa Denmark Martin Bille Herman ikulu jijini Dar es salaam.

Katika mazungumzo hayo wamejadili kuhusu uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Denmark huku wakigusia kuimarisha zaidi katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi miongoni mwa nchi hiyo.

Pia mazungumzo hayo yamehudhuriwa na balozi wa Denmark nchini Einar Hebogard pamoja na waziri wa fedha na mipango Phillip Mpango leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa wakizungumza masuala ya Afrika Mashariki kuhusu mgogoro wa Burundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *