Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na mmiliki wa kiwanda cha saraji cha Dangote kilichopo Mtwara, Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo Rais Magufuli amemuhakikishia mfanyabiashara huyo kwamba Serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini ili kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda.

Pia Rais Magufuli amesema kuwa katika kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara hapakuwa na tatizo lolote isipokuwa kuna watu walitaka kujinufaisha binafsi kupitia mradi huyo kwa kufanya biashara za ujanja ujanja.

Vile Magufuli amemtaka mfanyabiashra huyo kununua gesi moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya kutumia watu ambao walikuwa wanatengeneza faida.

Kwa upande wake mmiliki wa kiwanda hicho, Alhaj Dangote amesema kuwa ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amefunga kiwanda hicho kwa sababu amekatazwa kuingiza makaa ya mawe nje ya Tanzania kitu ambacho ameseka akiingi akilini kutoka na makaa ya mawe ya Tanzania yana ubora na raisi kupatikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *