Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) na kuagiza mali na shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na CDA zihamishiwe Halmashauri ya Manispaa Dodoma.

Rais Magufuli amesema uamuazi kwa kuivunja Mamlaka hiyo ni kutokana na kutaka kuhamishia majukumu yake katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.

Sababu nyingine ya kuvunjwa kwa mamlaka hiyo ni kuondoa mkanganyiko wa utoaji wa huduma kwa wananchi uliokuwa ukisababishwa na mgongano kati ya vyombo hivyo viwili na pia kuendana na mahitaji ya sasa ambayo yamedhidhirisha kuwa hakuna haja ya kuwepo kwa CDA.

Kufuatia kuvunjwa kwa mamalaka hiyo, Rais Magufuli pia ameivunja bodi ya CDA na aliyekuwa mkurugenzi wa CDA, Mhandisi Paskasi Muragili atapangiwa kazi nyingine hapo baadae.

Pia Rais Magufuli ameagiza kuwa wafanyakazi wote wa mamlaka hiyo wahamishiwe Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma na ofisi nyingine za serikali kadri inayowezekana.

Rais Magufuli pia ameagiza kuwa hati zote za kumiliki ardhi zilizotolewa na CDA kwa ukomo wa miaka 33 sasa ibadilishwe na kufikia ukomo wa umiliki wa miaka 99.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *