Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli amesema kuwa bado ataendelea kuchomoa baadhi ya watu katika vyama vya siasa nchini huku akisema ataacha vilaza tu kwenye vyama hivyo.

Rais Magufuli amesema hayo jana  alipokuwa kwenye ziara mkoani Tabora katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi.

Amesema kuwa maendeleo ya nchi hayana vyama ndiyo maana ameweza kuchangua baadhi ya viongozi kutokea upinzani na kudai kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo amesema kuwa Rais Magufuli amevunja mwiko wa Serikali kuwa ikiongozwa na watu kutoka chama kimoja baada ya kumteua yeye kuwa Katibu Mkuu wa Maji pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Anna Elisha Mghwira ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *