Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemteua mhandisi Emmanuel Karosso kuwa mwenyekiti wa kampuni ya ndege nchini (ATCL) kuanzia Septemba 15 mwaka huu.

Kabla ya uteuzi huo mhandisi Karosso alikuwa meneje wa TANROADS Musoma ambapo uteuzi huo ni wa miaka mitatu.

Pia Rais Magufuli amemteua Mhandisi Ladislaus Evarist Mtindi kuwa mkurugenzi mpya wa kampuni ya ndege (ATCL) ambapo nae uteuzi wake umeanza toka septemba 15 mwaka huu.

Kabla ya uteuzi huo mahandisi Mtindi alikuwa mkurugenzi wa EGNOS – Africa Joint Programme akishughulikia masuala ya anga katika ukanda wa Afrika.

                                         1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *