Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jonh Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbali mbali akiwemo Mkuu wa chuo kikuu cha Ardhi.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es salaam inasema Rais Magufuli amemteua Prof. Evaristo Liwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, kuchukua nafasi ya Prof. Idrissa B. Mshoro ambaye amestaafu.

Wakati huo huo Rais Magufuli amewateua Prof. Abdulkarim Khamis Mruma kuwa Mwenyekiti wa kampuni ya kuhifadhi mafuta (TIPER), ambaye kabla alikuwa ni Mtendaji Mkuu wa wakala wa Jiologia Tanzania.

Mwingine ni Prof. Joseph Buchweshaija ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania LTD.

Prof. Buchweshaija alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *