Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo anaendelea na ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani.
Rais Magufuli leo anatarajiwa kuzindua kiwanda cha matrekta kilichojengwa mkoani humo katika wilaya ya Kibaha.
Pia Rais Magufuli katika ziara yake hiyo atazindua barabara ya Bagamoyo – Msata pamoja na mradi wa maji wa Ruvu.
Akiwa katika ziara hiyo Rais Magufuli pia atazungumza na wananchi wa mkoa huo kuhusu maendeleo ya mkoa pamoja na taifa kwa ujumla.
Rais Magufuli amewasili katika mkoa jana na kuhutubia mamia ya watu katika uwanja wa Bwawani wilayani Kibaha.