Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameviagiza vyombo vya dola kufanya doria katika bahari ya India ili kudhibiti uvuvi haramu ambao umekuwa ukiathiri uchumi wa mkoa wa Pwani na taifa zima la Kenya.

Rais Uhuru amesema licha ya Kenya kuwa na hazina kubwa ya samaki katika eneo la Bahari ya Hindi hainufaiki chochote kutokana na uvuvi haramu unaofanywa na baadhi ya watu.

 

Pia amesema kuwa watu wa Kenya wanahitaji ajira wakati sekta ya uvuvi ikihujumiwa na mataifa mengine hivyo basi ni lazima uvuvi haramu usitishwe ili kuwawezesha vijana wa Kenya kufanya uvuvi ili kuboresha uchumi wa nchi.

 

Rais huyo amewataka raia wa nchi hiyo kushirikiana na Serkali ya nchi hiyo ili kupiga vita uvuvi haramu katika maeneo ya mji wa Mombasa nchini Kenya.

 

Uvuvi haramu ni janga kubwa ukanda wa Afrika Mashairiki ambapo wavuvi hao haramu hutumia mabomu kuvulia samaki pamoja na kutumia nyavu zenye tundu ndogo ambazo zimepigwa marufuku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *