Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema kuwa yupo tayari kurejea uchaguzi baada ya mahakama ya juu nchini humo kutengua ushindi wake.
Kenyatta amesema amekubali uamuzi wa Mahakama licha ya kwamba hajaafikiani na Majaji sita waliohusika kutoa maamuzi hayo.
Pia amesema kuwa haiwezekani raia zaidi ya milioni 40 wa Kenya waliochagua chama chake cha Jubilee maamuzi yao yaje yatenguliwe na watu sita pekee.
Kwa upande mwinigine Rais Kenyatta amewataka wananchi wa Kenya kuendelea kuwa wamoja na kutokaribisha tofauti zao, akisema umoja ndiyo nguzo muhimu kwa taifa hilo.
Mahakama ya Juu nchini Kenya imetengua matokeo ya uchaguzi uliofanyika Agosti 8 mwaka huu ambao ulimpa ushindi Rais Kenyatta kwa kusema ulikuwa na dosari, na uchaguzi utarudiwa kwa mara ya pili ndani ya siku 60.