Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Dk John Pombe Magufuli leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya siku ya mashujaa nchini ambapo kitaifa yanafanyika mkoani Dodoma.

Akiongea na waandishi wa habari mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordani Rugimbana amesema maadhimisho hayo yatafanyika katika uwanja wa mashujaa leo kuanzia asubuhi na mgeni rasmi atakuwa Rais John Pombe Magufuli.

Katika Mahadhimisho ayo kutakuwa na matukio mbali mbali kama gwaride la maombolezo kutoka vikosi vya majeshi ya kujenga taifa na jeshi la wananchi pamoja na uwekaji wa taji la maua katika mnara, silaha za asili na upigaji wa mizinga.

Mkuu wa mkoa huyo amewataka wakazi wa dodoma kutoka sehemu mbali mbali kujitokeza katika viwanja vya mashujaa ili kushiriki katika maadhimisho hayo, huku akitoa shukrani wa Serikali kuupa heshima mkoa wa Dodoma ambao ni makao makuu ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *