Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amelihutubia taifa baada ya kuwa Uingereza kwa miezi mitatu akipata matibabu.

Raia wengi wa Nigeria walimwomba ajiuzulu wakati hakuwepo nchini wakisema hakuwa na uwezo wa kuiongoza nchi.

Wengine wamemuuliza kusema anaugua nini huku uvumi ukiongezeka kuhusu uwezekano wake kuwania urais tena mwaka 2019.

Makamu wa Rais Yemi Osinbajo amekuwa akiwajibika wakati Buhari amekuwa Uingereza, lakini Buhari sasa amerejea kazi yake kama rais.

Rais pia alizungumzia vita vya kikabila nchini akisema vinasababishwa na wahalifu wa kisiasa nchini humo.

Kuna watu ambao wamekuwa wakiitisha kuanzishwa kwa nchi tofauti maeneo ya kusini-mashariki inayojulikana kama Biafra huku vita dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu, Boko Haram vikiendelea katika maeneo ya kaskazini.

Raia wa Nigeria walikuwa wanatumai kupata habari kuhusu kile kinachomfanya rais wao kuugua lakini ofisi ya rais imekataa kufichua lolote.

Licha ya kuwa imesisitizwa kuwa Buhari yuko sawa na mwenye afya, alionekana mnyonge akiwasalimia wanasiasa jumamosi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *