Ombi la utawala wa mkoa kwa ajili ya mazishi ya kiserikali kwa mwanamuziki maarufu wa Afrika Kusini aliyeuawa wiki iliyopita limekataliwa na rais, vinaripoti vyombo vya habari vya ndani.

Waziri Mkuu wa Gauteng Panyaza Lesufi alikuwa amemwandikia Rais Cyril Ramaphosa akiomba ruhusa ya kumpa rapa aliyeuawa Kiernan Forbes, maarufu kama AKA, mazishi ya kitaifa

Mnamo Alhamisi, Bw Lesufi alisema ombi lake lilikataliwa.

Alisema hakuomba fedha za serikali kwa ajili ya mazishi, bali jeneza lifunikwe bendera ya taifa na bendera kupeperushwa nusu mlingoti kwa heshima ya rapa huyo.

“Tulihisi kwamba mtu wa hadhi yake ya kimataifa, mtu wa hadhi ya kitaifa, lazima kuwe na aina fulani ya heshima, na tunataka kufafanua sio mchango wa kifedha,” alinukuliwa akisema.

Familia ya rapa mkubwa nchini Afrika Kusini aliyeuawa kwa kupigwa risasi, Kiernan Forbes almaarufu AKA imetoa taratibu za mazishi za staa huyo ambaye atazikwa Februari 18, 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *